Mchezaji wa Manchester City, Kalvin Phillips anatarajiwa kupewa ofa ya kurudishwa katika kikosi chake cha zamani cha Leeds United msimu ujao.

Phillips, anayekipiga kwa mkopo katika timu ya West Ham akitokea Manchester City huenda akarejea katika kikosi chake cha zamani kama wakifikia mwafaka pande zote mbili.

Staa huyo alisajiliwa na Manchester City mwaka 2022 ambapo alicheza mechi 16 pekee na kutolewa kwa mkopo kwenda kuongeza kiwango chake katika timu ya West Ham.

Taarifa iliyotoka katika mitandao ilisema Phillips atarejea Manchester City mwishoni mwa msimu huu ambapo uongozi wake umepanga kumrudisha Leeds United.

Taarifa zaidi zilisema kuwa kiungo huyo alilazimika kutolewa kwa mkopo kutokana na kushindwa kuonyesha kiwango bora chini ya Kocha Pep Guardiola.

“Phillips anatarajia kurejea Manchester City mwishoni mwa msimu huu ambapo uongozi umepanga kumrudisha katika timu yake ya zamani ya Leeds United kufuatia kushindwa kuonyesha kiwango bora,” ilisema taarifa hiyo.

Phillips anatarajiwa kupelekwa Leeds United kwa dau la pauni milioni 30 katika msimu ujao.

Sergei Palkin: Chelsea hawajui kumtumia Mudryk
Rais Samia kutunukiwa Udaktari wa heshima Uturuki