Malkia Elizabeth wa Uingereza, amemkabidhi rasmi Theresa May majukumu mawili makubwa ya nchi hiyo ya kuwa Waziri Mkuu na Muidhinishaji Mkuu wa fedha za nchi hizo.
Theresa anakuwa mwanamke wa pili katika historia ya nchi hiyo kushika wadhifa wa Waziri Mkuu baada ya Margaret Thatcher aliyeacha historia kubwa ya utawala wake.
Waziri Mkuu huyo mpya amechukua hiyo baada ya David Cameron kujiuzulu nafasi hiyo wiki chache zilizopita baada ya Uingereza kupiga kura ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.
Tayari ameshaunda Baraza la Mawaziri wake ambao wameanza kuelezea vipaumbele vyao tangu jana.