Kundi la kigaidi linalojiita Islamic States (IS) limesambaza picha za mtu aliyejitoa mhanga na kulipua basi lililokuwa limewabeba walinzi wa rais wa Tunisia, Jumanne wiki hii.

Basi hilo lililolipuliwa mbele ya hotel moja na kuchukua uhai wa walinzi 13 wa rais pamoja na mshambuliaji huyo.

Kundi hilo limemtaja mshambuliaji huyo kwa jina la Abu Abdullah na kwamba aliweza kutekeleza shambulio hilo baada ya kuliingilia gari hilo. Picha hiyo pia imewekwa kwenye mtandao wa Twitter na mchambuzi wa masuala ya kiusalama, Micheal Horowitz.

Mshambuliaji

Katika picha hiyo, kundi hilo limeambatanisha ujumbe wa vitisho likieleza kuwa hawataacha kuishambulia Tunisia hadi ‘sharia’ itakapoanza kutumika nchini humo.

Kutokana na tukio hilo, rais wa Tunisia ametangaza hali ya tahadhari kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Magufuli afuta sherehe Siku ya Ukimwi Duniani
Viongozi waliowahi kuiba mali za Umma wajisalimisha kwa Rais