Klabu ya Manchester United imeripotiwa kushika nafasi ya tano kwa utajiri duniani, kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Kwa nafasi hiyo Man Utd wamepanda kwa asilimia saba tofauti na orodha ya mwisho iliyotolewa na jarida hilo.

Klabu ya mchezo wa American Football, Dallas Cowboys ndio inayoongoza kwenye orodha hiyo kwa kuwa na thamani dola bilioni 4 ambazo ni sawa na Pauni ya Uingereza bilioni 3.03, na ni mara ya kwanza kwa klabu ambayo haichezi soka kuongoza kwenye orodha hiyo tangu kuanzishwa kwake 2011.

Man Utd, walioongoza orodha hiyo mwaka 2011 na 2012, kwa sasa wana thamani ya dola bilioni 3.32 ambazo ni wasa na Pauni bilioni 2.52.

Real Madrid ni wa pili kwa kuwa na thamani ya dola bilioni 3.65 sawa na Pauni bilioni 2.77 na Barcelona wa tatu wakiwa na thamani ya dola bilioni 3.55 sawa na Pauni bilioni 2.69.

Man Utd ambayo ni klabu pekee ya England katika orodha hiyo, imesaidiwa sana na mkataba wa Pauni milioni 750 walioingia na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas, jambo ambalo lililoongeza thamani yao licha ya kushindwa kufuzu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2016-17.

Hata hivyo, Manchester Utd, ndio wenye deni kubwa zaidi miongoni mwa klabu zilizo katika orodha ya 25 bora iliyotolewa na jarida la Forbes.

Klabu nyingine za England zilizopo kwenye orodha hiyo ni Arsenal (23), Manchester City (28), Chelsea (36) na Liverpool (41).

Na hii ndio kumi bora ya klabu za michezo tajiri duniani kwa mujibu wa gazeti la Forbes la Marekani.

  1. Dallas Cowboys $4bn (£3.03bn)
  2. Real Madrid $3.65bn (£2.77bn)
  3. Barcelona $3.55bn (£2.69bn)
  4. New York Yankees $3.4bn (£2.58bn)
  5. Manchester United $3.32bn (£2.52bn)
  6. New England Patriots $3.2bn (£2.43bn)
  7. New York Knicks $3bn (£2.27bn)
  8. Washington Redskins $2.85bn (£2.16bn)
  9. New York Giants $2.8bn (£2.12bn)
  10. Los Angeles Lakers $2.7bn (£2.05bn)

Muhimu: $ ni dola ya Marekani na £ Pauni ya Uingereza

Kituo cha Polisi Kapenguria Kenya Chavamiwa
Ni noma kufanya Mapinduzi ya Filamu Nchini- Lulu