Kumekuwa na tetesi mitandaoni zikimuhusisha kiungo bora katika klabu ya Kaizer Chiefs na ligi ya Afrika Kusini Anthony Akumu Agai kutua Young Africans wakati wa dirisha dogo.

Tetesi hizo zilianza tangu msimu uliopita wakati kiungo huyo kutoka nchini Kenya alipokuwa na klabu ya Zesco Utd ya Zambia, kabla ya kujiunga na klabu ya Kaizer Chiefs.

Akumu mwenye umri wa miaka 28, alikua sehemu ya wachezaji waliotajwa kuwania na Young Africans sambamba na akina Kisinda, Mukoko na James Kotei.

Tetesi hizi zilirudi tena mapema juma hili, baada ya Mhandisi Hersi Said kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kumuwish birthday Akumu na watu kutafsiri moja kwa moja kuwa huenda akasajiliwa na Young Africans wakati wa dirisha dogo.

Hata hivyo mkuu wa idara ya habari na mawasilino ya Young Africans Hassan Bumbuli amekanusha tetesi hizo kwa kusema: “Hersi Said ana marafiki wengi kama mtu mwingine akiwemo akumu, kumuwish birthday sio kwamba ndo tayari tumeshamsajili”

“Lakini Young Africans bado tuna nafasi moja ya kusajili mchezaji wa kigeni tunaweza kumsajili yeyote, wasubiri mwalimu atatoa mapendekezo gani” amesema Bumbuli.

Serikali ya Nigeria yatangaza marufuku ya kutoka nje
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 23, 2020

Comments

comments