Msanii wa muziki bongo, Ali Saleh Kiba maarufu kama King Kiba amesema kuwa wimbo wake wa ‘Hela’ alioutoa ni maalumu kwa marehemu dansa wake Emmanuel Elias ambaye aliwahi kufanya nae kazi

Ameongezea kuwa dansa huyo ndiye aliyetunga staili ya kucheza kwenye nyimbo hiyo iliyotungwa 2013 na kutolewa rasmi jana Oktoba 4, 2018.

Hivyo Alikiba amesema ameuachia wimbo huo kwa heshima ya marehemu Emmanuel.

”Hela ni wimbo maalum kwa ajili ya kumuenzi marehemu Emmanuel Elias, ambaye niliwahi kufanya naye kazi kama ‘dancer’ wangu. Alikuwa anaupenda huu wimbo sana na alikuwa anaucheza wakati wa dance rehearsals zetu . Huu wimbo ni dedication kwake. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi” ameandika Kiba kwenye ukurasa wake wa You Tube na kuitambulisha kuwa nyimbo hiyo siyo rasmi bali ni ya kumuenzi marehemu dansa yake, ”Unofficial Dedication Release Music Video).

“Nilliifanya nyimbo ya hela zamani sana kama 2013, sasa hivi nataka kuichaia kwa sababu dancer wangu Emmanuel ndiye aliitungia style ya kucheza akawafundisha wenzake wote, bahati mbaya Mungu alimpenda alifariki, na niliwaahidi dancers ambao walikuja kwenye msiba kwamba nitafanya nyimbo kwa sababu Ima alisimamia nyimbo ya hela kwa kiasi kikubwa sana, ahadi yangu nilitaka niitimize kwenye arobaini yake ambayo imepita hivi juzi”, amesema Alikiba alipohojiwa na kituo cha EATV.

Hata hivyo Alikiba amesema kwamba kwenye video ya wimbo huo ameweka picha za dancer huyo ambaye kwa sasa ni marehemu, kama kumpa heshima yake.

Video: Mbunge Neema amwaga misaada Njombe
Mdee: Hakuna anayeomba kujiunga CCM, ni uoga