Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amewajibu baadhi ya mashabiki wanaompinga  kwa kuwaambia, mustakabali wake hautategemea kufaulu kwa kikosi chake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.

Wenger ametoa kauli hiyo, kufuatia shinikizo la mashabiki wanaompinga katika kipindi hiki kwa kumtaka aondoke klabuni hapo mara mkataba wake utakapokwisha  mwishoni mwa msimu huu, kwa kuamini uwezo wake wa kufundisha soka umeporomoka.

Mashabiki hao wanaamini kuporomoka kwa Arsenal hadi katika  nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ya nchini England, huenda kukasaidia mpango wa kuondoka kwa mzee huyo ambaye karibu misimu yote amekua akikiwezesha kikosi chake kumaliza katika nafasi nne za juu.

Inaaminika huenda mafanikio ya kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi ya England, ndio yanampa jeuri meneja huyo mbele ya viongozi wa Arsenal kwa kuamini katu hawezi kutimuliwa hata kama ataendelea kuukosa ubingwa EPL.

Ushindi wa mabao matatu kwa moja wa Man utd dhidi ya Middlesbrough uliishusha rasmi Arsenal hadi katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ya England hapo jana, baada ya The Gunners kukubali kufungwa dhidi ya West Bromwich Albion  mabao matatu kwa moja siku ya Jumamosi.

“Maamuzi yangu hayatategemea nafasi tutakayoipata kwenye msimamo wa ligi mwishoni mwa msimu huu, tumewahi kumaliza katika nafasi nne za juu kwa miaka 20 iliyopita, na mambo mengine yaliendelea”

“Nimefanya kazi kubwa sana katika klabu hii, na muda si mrefu nitachukua maamuzi ya mustakabnali wangu.” Alisema mzee huyo wa miaka 67.

Arsenal imekua na wakati mgumu wa kupata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa England tangu mwaka 2004, hali ambayo inaendelea kuwatia machungu mashabiki wa klabu hiyo.

Bristol whos who online registry review
Marco Verratti Kubaki Parc des Princes