Kikosi cha AS Vita Club kinatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam, Tanzania leo Alhamisi Aprili Mosi, kikitokea kwao DR Congo kupitia Addis Ababa,Ethiopia kwa ndege ya Shirikika la Ndege la Ethiopia.

AS Vita Club itawasili nchini tayari kwa mchezo wa mzunguuko wa tano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi dhidi ya Simba SC, utakaochezwa Jumamosi (April 03) Uwanja wa Benjamin Mkapa  jijini Dar es salaam.

Hata hivyo kikosi cha klabu hiyo ya mjini Kinshasa huenda kikawakosa wachezaji wawili wa kikosi cha kwanza, Ernest Luzolo na Djouma Shabani.

“Luzolo na Shabani wote waliumia katika katika timu ya taifa ya Congo na majeraha waliyoyapata ni makubwa ambayo yanaweza kuwaweka nje si chini ya miezi sita,”

“Wachezaji hao hawatakuwepo kutokana na majeraha makubwa ambayo wameyapata wakiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya DR Congo”.

“Hawawezi kuwepo kwani majeraha ambayo wameyapata wanaweza kuwa nje ya uwanja hata kwa mwaka mmoja,” amesema Nestor Mutuale  ambaye ni wakala mkubwa wa wachezajinchini DR Congo.

Mutuale ndio wakala ambaye amewaleta nchini, wachezaji watatu, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda wote wa Yanga pamoja na Mpiana Monzinzi.

Wateule wa Rais Samia kuapishwa leo
Uwaziri ni cheo cha muda - Ndugai