Mchezo wa michuano ya kombe la Mapinduzi, uliokua unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini kote, kati ya Azam FC dhidi ya Dar es salaam Young Africans umemalizika kwa sare ya bao moja kwa moja huko visiwani zanzibar.

Mchezo huo wa hatua ya makundi umechezwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, usiku huu, ulikua na ushidani mkubwa huku ukitawaliwa na ubabe wa hapa na pale.

Azam FC ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Kipre Tchetche katika dakika ya 56 baada ya mabeki wa Yanga kujipanga vibaya na mfungaji akavunja mtego na kuuwahi mpira kabla ya kupiga shuti kali lililomzidi Deo Munishi ‘Dida’.

Yanga nao waliendelea kupambana na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 82 kupitia kwa Donaldo Ngoma baada ya makosa ya kipa Aishi Manula ambaye alidaka mpira na kuudondosha.

Bao la Yanga lilipatikana dakika chache baada ya nahodha wa Azam FC, John Bocco kulambwa kadi ya pili ya njano iliyozaa kadi nyekundu.

Kila timu imecheza mechi ya pili, Azam FC ikifikisha pointi mbili baada ya sare ya kwanza ya mabao 2-2 dhidi ya Mtobwa Sugar, huku Yanga ikifikisha pointi 4 baada ya kuanza michuano hiyo kwa ushindi.

 

Zitto Aishangaa serikali kulilea jipu hili
Pep Guardiola Avunja Ukimya, Asema Wapi Atakapoelekea