Tangu video ya ‘chura’ ya msanii Snura kufungiwa na Serikali ni miezi  kadhaa sasa na leo kuna hii story kuwa msanii huyo amewasilisha script bodi ya filamu kwa ajili ya kuifanyia video nyingine.

Mtendaji wa Bodi ya filamu nchini Joyce Fisso amesema kuwa Snura aliwasilisha script ndogo kwaajili ya kuitengeneza tena lakini ilikuwa haijawa na muelekeo, haijawa tofauti na ile ya zamani, haina maudhui na haikufafanua anataka hasa kupeleka ujumbe gani kwa jamii.

”Snura aliwasilisha script ndogo kwa ajili ya kuitengeneza tena, hata hii aliyoileta bado ilikuwa na muelekeo huo, haikuwa na tofauti na ile ya mwanzo, haikuwa na maudhui na haikufafanua hasa anataka kupeleka ujumbe gani kwa jamii’’ – Joyce Fisso

Joyce ameongea hayo kupitia Millard Ayo, pia ameongezea kwa kusema mhusika anayo haki ndani ya siku 30 toka maamuzi yametolewa kukata rufaa kwa Waziri mwenye dhamana.

kamati haijaridhia ile script yake kwenda kutengenezea video, mhusika anayo haki ndani ya siku 30 toka maamuzi yametolewa kukata rufaa kwa Waziri mwenye dhamana lakini jana tumepokea barua ameleta script nyingine amesema amefanyia marekebiso bado tunaifanyia kazi” – Joyce Fisso

Video: Serikali imeyakubali haya mapendekezo ya Mbunge Bashe
Fredrick Kitenge: Yanga Ni Wachanga Mno Kushindana Na TP Mazembe