Kocha Hans van der Pluijm ananukia Azam Complex, kufuatia uongozi wa Azam FC kuonyesha nia ya kumpa nafasi.

Bado hakujawa na muafaka kwa kocha huyo kutoka nchini Uholanzi, achukue nafasi ya kocha mkuu au mkurugenzi wa Ufundi.

Pluijm ametangaza kujiuzulu Yanga baada ya Kocha George Lwandamina kutua nchini na kumalizana na uongozi wa klabu hiyo kongwe.

Baada ya kumaliza taratibu za kusaini mkataba wa kufanya kazi na Yanga, Lwandamina anatarajiwa kurejea nchini kwao Zambia kabla ya kutua tena Dar es salaam kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.

Lakini Azam FC wameonyesha nia ya kumnasa Pluijm ambaye waliwahi kumuwania hapo awali.

“Kuna mazungumzo ingawa inafanywa siri kubwa, sijajua sahihi ni mkurugenzi wa ufundi au kocha mkuu.

“Nafikiri ni suala ambalo linaendelea kushughulikiwa,” kilieleza chanzo.

Kumekuwa na ugumu kuwapata viongozi wa Azam FC lakini juhudi zinaendelea ili kupata kauli yao kuhusiana na Pluijm pia Kocha Zeben Hernandez raia wa Hispania ambaye anakinoa kikosi chao.

Mauricio Pochettino: Moussa Sissoko Alimpiga Arter Kwa Makusudi
Atletico Madrid Yang'ara Tuzo Za La Liga 2015-16