Mshambuliaji kutoka nchini Italia, Super Mario Barwuah Balotelli, amedhihirisha mapenzi yake na klabu ya AC Milan licha ya kusajiliwa kwa mkopo akitokea Liverpool, mwishoni mwa usajili wa majira ya kiangazi.

Balotelli amedhihirisha mapenzi na klabu hiyo ya mjini Milan, baada ya kupiga picha ya kuianika hadharani kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, ambapo ameoneoakana akiibusu nembo ya The Rossoneri.

Kama hilo halikutosha, Balotelli ameandika maandishi yaliyoambatana na picha hiyo kwa kusisitiza anaipenda sana AC Milan zaidi ya ilivyokua siku za nyuma wakati akiwa klabuni hapo kabla ya kuuzwa huko Anfield mwezi August mwaka 2014.

Balotelli, bado hajabahatika kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza cha AC Milan katika michezo ya ligi ya nchini Italia, zaidi ya kucheza mchezo uliowashirisha wachezaji wa akiba wakati wa mchezo dhidi ya Empoli ambapo alibahatika kufunga bao lililoipa ushindi timu yake wa mabao mawili kwa moja.

Hata hivyo kuna uwezekano akacheza mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo AC Milan watawakabili Inter Milan kwenye uwanja wa San Siro.

Mayweather Atoa Sababu Za Kumkataa Amir Khan
Niko Kovac Afungashiwa Virago Croatia