Wizara ya mambo ya nje ya Italia imesema kuwa balozi wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ameuawa katika shambulio dhidi ya msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa mashariki mwa nchi hiyo.

Katika shambulio hilo lililotokea karibu na mji wa Kanyamahoro Balozi Luca Attanasio wa Italia nchini DRC, mwanajeshi mmoja wa Italia na dereva wa gari ambaye ni raia wa Congo wameuawa.

Maafisa katika mbuga ya wanyama ya Virunga wanasema shambulio hilo lilikuwa jaribio la utekaji nyara.

Makundi mengi yaliyojihami yanaendesha harakati zake karibu na mbuga hiyo inayopakana na Rwanda na Uganda.

Walinzi wa mbuga hiyo wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara na kuuawa na waasi.

“Ni kwa masikitiko makubwa kwamba wizara ya mashauri ya kigeni inathibitisha, kifo leo, mjini Goma, cha balozi wa Italia ,” taarifa ya wizara ilisema.

Watu wengine walwili waliouliwa walikuwa ni askari polis mwenye umri wa miaka 30 Vittorio Iacovacci, ambaye amekuwa akihudumu katika ubalozi tangu mwezi septemba mwaja jana, na dereva wao raia wa Congo, ambaye jina lake bado halijatangazwa rasmi.

Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi ametoa taarifa yake ya “rambi rambi kubwa”, huku Rais Sergio Mattarella akilaani shambuli hilo.

Sauko: Simba SC msitembee na matokeo mkononi
Bobi Wine aondoa kesi ya kupinga matokeo mahakamani