Mchezaji raia wa Tanzania Abdi Banda anayecheza nchini Afrika Kusini amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu yake ya  Highlands Park inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo.

Banda ambaye anacheza nafasi ya mlinzi wa kati mshahara wake utakuwa ni rand 150,000  ambazo ni zaidi ya Sh Milioni 24 za Kitanzania.

Kabla ya kusaini ‘dili’ hilo, Banda alikuwa anakipiga Baroka FC ya Afrika Kusini ambayo aliachana nayo baada ya mkataba wake kumalizika.

Ikumbukwe beki huyo kabla ya kutua Baroka  alikuwa akiichezea Simba SC ambayo ilimsajili kutokea Coastal union ya Tanga.

Disemba 31 laini zote zisizosajiliwa kufungwa, NIDA, TCRA waungana kufanya usajili
Dalali awapigia chapuo Chilunda, Naddo Azam Fc