Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Karim Mostafa Benzema ameendelea kuwatia simanzi mshabiki wa klabu ya Arsenal kwa kuwaarifu jambo la kutokua na mpango wa kuihama klabu yake kwa sasa.

Benzema, kwa kipindi cha majuma kadhaa amekua akihusishwa na taarifa za kuwa mbioni kusajiliwa na klabu ya Arsenal akitokea Estadio Santiago Bernabeu pale mjini Madrid nchini Hispania.

Benzema aliwaarifu mashabiki wake na wale wa The Gunners kwa kuandika kwenye akauti yake ya ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter, hana mpango wa kuondoka Real Madrid na kusaka mahala pengine pa kusaka rizki yake.

Tetesi za kuondoka kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, zilianza kuibuliwa mara baada ya kuachwa kwenye kikosi cha Real Madrid kilichokwenda kufanya ziara ya maandalizi ya msimu wa ligi huko mashariki ya mbali mwezi uliopita.

Tetesi ziliendelea kupewa mkazo mkubwa mwishoni mwa juma lililopita, baada ya Benzema kutokuwepo kwenye kikosi cha Real Madrid ambacho kilipambana kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya nchini Hispania dhidi ya Sporting de Gijón ambao walilazimisha matokeo ya sare ya bila kufungana.

Stars Yaanza kuivutia Kasi Nigeria
FC Barcelona Kukosa Alves Kwa Mwezi Mzima