Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini imetaongeza fedha za mkopo kwa wanafunzi kwa awamu ya pili ambapo wanafunzi 40,836 wamepata mikopo hadi sasa.

Idadi hiyo imefkiwa jana baada ya Bodi hiyo jana imetoa majina 28,554 baada ya majina ya mwanzo ya wanafunzi 12,282.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Bodi hiyo, wanafunzi wenye sifa za kupata mkopo ni 50,830 hivyo wanafunzi waliobaki ni 10,094 ambapo Bodi hiyo imeahidi kuwapa mikopo katika awamu nyingine itakayotoka hivi karibuni.

Awali, wanafunzi wa elimu ya juu walianza kulalamikia Bodi hiyo kukosa mikopo ambapo Bodi hiyo iliahidi kutoa mikopo kwa wanafunzi hao kwa awamu.

“Hii Bodi ilianzishwa ili kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji wapate elimu ya juu na sio kuwafanya wasipate elimu ya juu,” alisema Afisa Habari wa Bodi hiyo, Omega Ngole.

Yametimia, David Moyes Hana Kazi Hispania
Dk. Shein Maalim Seif Wakutana Kumaliza Mambo