Hatimae meneja kutoka nchini Scotland, David Moyes ameonyeshwa mlango wa kutokea kwenye klabu ya Real Sociedad ya nchini Hispania, kutokana na mwenendo wa kazi zake kutowaridhishwa viongozi waliompa ajira mwaka mmoja uliopita.

Moyes mwenye umri wa miaka 52, alikabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi cha Real Sociedad,  Novemba 10, mwaka 2014, na alifanikiwa kukisogeza hadi kumaliza kwenye nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi ya nchini Hispania msimu uliopita.

Kwa msimu huu mambo yalionekana kuwa magumu kwa Moyes, kutokana na mbinu zake kugonga mwamba, hadi kufikia hatua ya klabu hiyo kuwa kwenye nafasi za chini katika msimamo wa ligi ya nchini humo.

Mwishoni mwa juma lililopita, Moyes alikishuhudia kikosi chake kikipoteza mchezo dhidi ya Las Palmas kwa kufungwa mabao mawili kwa sifuri, ikiwa ni mchezo wa nne kufungwa miongoni mwa michezo kumi na moja iliyochezwa mpaka sasa.

Kufutwa kazi kwa David Moyes ambaye alishindwa kuvaa viatu vya Sir Alex Ferguson huko Old Trafford miaka miwiwli iliyopita, kunamjumuisha hadi aliyekua msaidizi wake Billy McKinlay kuondolewa klabuni hapo.

Ajira ndani ya Real Sociedad ilikuwa ya kwanza kwa Moyes kuipata baada ya kufutwa kama meneja wa Manchester United, mwezi Aprili mwaka 2014 baada ya kuwaongoza kwa miezi 10 pekee.

Mkurugenzi wa Muhimbili Aandika Historia Kwa Rais Magufuli
Bodi Ya Mikopo Yaongeza Pesa Kwa Wanafunzi