Hali imeanza kuonesha matumaini visiwani Zanzibar baada mgombea urais kupitia CCM, Dk. Ali Shein na mgombea urais kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kukutana jana na kuteta kwa zaidi saa 4.

Taarifa kutoka visiwani humo zimeeleza kuwa mkutano kati ya Dk. Shein na Maalim Seif ulihudhuriwa na marais wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Hassan Mwinyi na Amani Karume.

Hata hivyo, bado haijaweka wazi kilichozungumzwa katika kikao hicho bado hayajawekwa wazi.

Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za kutafuta muafaka wa Zanzibar baada ya mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha kutangaza kufuta uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu kwa madai kuwa ulikuwa na kasoro nyingi hususan visiwani Zanzibar.

Bodi Ya Mikopo Yaongeza Pesa Kwa Wanafunzi
Patrick Vieira Ahamia Marekani