Kiungo wa Klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Sergio Busquets, amekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Busquets amekutwa na kadhia hayo baada ya kuiongoza kama nahodha timu ya taifa ya Hispania katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ureno uliopigwa Ijumaa na kumalizika kwa sare ya 0-0.

kiungo huyo amepata maambukizi hayo ikiwa ni siku chache kabla ya Kuanza michuano ya Euro Juni 11, 2021 lakini mchezo wao wa Kwanza wa Euro kwa timu ya taifa ya Hispania utapigwa Juni 14 dhidi ya Sweden.

Hispania imepangwa kundi E ambalo lina timu za mataifa ya Sweden, Poland na Slovakia.

Kocha mkuu wa Hispania Luis Enrique juma lililopita alitangaza kikosi cha wachezaji zaidi ya ishiriki ambapo upande wa MAKIPA yupo David de Gea (Manchester United), Unai Simon (Athletic Bilbao) na Robert Sánchez (Brighton & Hove Albion)

MABEKI

Aymeric Laporte (Manchester City), Jordi Alba (Barcelona), Jose Gaya (Valencia), Pau Torres (Villarreal), Diego Llorente (Leeds United), Eric García (Manchester City) na Cesar Azpilicueta (Chelsea)

VIUNGO

Sergio Busquet (Barcelona), Koke (Atletico Madrid), Marcos Llorenta (Atletico Madrid), Thiago (Liverpool), Rodri (Manchester City), Fabian (Napoli) na Marcos Llorente (Atletico Madrid)

WASHAMBULIAJI

Alvaro Morata (Juventus), Mikel Oyarzabal (Real Sociedad), Gerard Moreno (Villareal), Dani Olmo (RB Leipzig), Pedri (Barcelona), Ferran Torres (Manchester City), Adama Traore (Wolverhampton Wanderers) na  Pablo Sarabia (Paris Saint-Germain).

Michango ya shule ni hiari wazazi wasilazimishwe - Silinde
Milioni 100 kung'oa Makambo Horoya AS