Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wananchi kupuuzia wito unaotolewa na viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda ngome ya Ukawa wa kuwataka wananchi hao kulinda kura zao vituoni baada ya zoezi la kupiga kura.

Akihutubia umati mkubwa uliohudhuria mkutano wa hadhara katika jiji la Mwanza, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amewaeleza wananchi hao kuwa kamwe wasikubali kubaki vituoni kulinda kura kwa kuwa kazi ya ulinzi ni jukumu la Jeshi la polisi, na uangalizi wa kura ni jukumu la mawakala wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki.

“Kulinda kura ni kazi ya vyombo vya ulinzi na usalama, kazi ya kusimamia kura kwenye vituo ni ya vyama vya siasa. Kila chama cha siasa kina wakala. Na mule ndani ya chumba cha kupigia kura, CCM wanamtu mmoja tu, waulizeni wao wana wangapi? Anayekwambia nenda kalinde kura, mwambie mzee naomba tulinde pamoja,” Alisema Kinana.

Viongozi wa Ukawa wamekuwa wakiwahimiza wananchi kuhakikisha wanalinda kura zao mara baada ya zoezi la kupiga kura kwa kukaa umbali wa mita 100 kutoka katika vituo husika kwa madai kuwa CCM ina historia ya kuiba kura za vyama vya upinzani.

 

UEFA Wabariki Adhabu Ya Bosi Wao
Kinana Hamuachii Lowassa, Hakumbuki Chochote…