Kituo cha Kutafiti na Kudhibiti Maradhi (CDC) kimethibitisha kuongezeka kwa dalili sita mpya za virusi vya corona zinazoweza kuonekana kuanzia siku ya pili hadi siku ya 14 mtu anapokuwa amepata maambukizi.

Kimetaja dalili hizo kuwa ni baridi, maumivu ya misuli, maumivu ya kichwa, maumivu ya koo, kutetemeka, Kupoteza ladha na uwezo wa kunusa.

“Tunaweza kusema kuwa dalili hizi sita zinaambatana na COVID-19,” CDC ilisema.

Hata hivyo aliyekuwa Afisa Mkuu Mwandamizi katika ofisi ya majanga chini ya utawala wa rais Barack Obama, Mario Ramirez, aliambia Washington Post kuwa dalili za ugonjwa huo mpya hubadilika kila mara.

Na kwamba dalili hizo zilichunguzwa kupitia kwa wagonjwa wengi nchini Marekani na pia utafiti kutoka kwa mataifa mengine.

Ambapo utafiti uliofanywwa kwa wagonjwa bara Uropa ulifichua kuwa kati ya 86% na 88% miongoni mwao waliripoti dalili za kupoteza ladha na hisia ya kunusa.

Huku utafiti wa Iran kwa upande mwingine ulionyesha 76% ya wagonjwa wa COVID-19 walipoteza uwezo wa kunusa.

Yvonne Mugure, ambaye ni mmoja wa Wakenya mwenye umri wa miaka 30 ambae alipatwa na COVID-19 nchini Marekani alisema alipoteza hisia za kunusa baada ya kuambukizwa ugonjwa huo hatari.

“Kitu cha kwanza ambacho nilitambua ni kukosa kunusa. Wakati nilikuwa nakula chakula niligundua hakikuwa na ladha. Nilipuuza nikidhania kuwa chakula hakikuwa kimepikwa vizuri lakini wakati niliamka kwenda kuketi nilihisi kitu kikininyonga na kuamua kwenda hospitali,” amesema Mugure.

Aidha hapo awali dalili zilizokuwa zinaripotiwa kuwa ni za ugonjwa wa COVID 19 ni pamoja na homa kali na kujihisi kuchoka, kukohoa, kupata shida wakati wa kupumua pamoja na kuumwa kwa misuli.

Rwanda: 1,673 waachiwa kutoka gerezani kupambana na corona
Mgunduzi wa barakoa arudi kazini baada ya kustaafu