Nahodha wa zamani wa timu ya kriketi ya West Indies, Chris Gayle amepigwa faini baada ya kuthibitika alimtongoza mwanahabari wakati wa mahojiano ya moja kwa moja.

Gayle amepigwa faini ya dola 10,000 za Australia (sawa na $7,200; £4,900) na klabu yake ya Melbourne Renegades inayocheza ligi ya Big Bash.

Mchezaji huyo alimuuliza mwanahabari wa kipindi cha Ten Sport, Bi Mel McLaughlin kama wangeweza kwenda ‘date’ alipokuwa akihojiwa wakati wa mechi ya ligi dhidi ya Hobart Hurricanes Jumatatu.

“Kuyatazama macho yako mara ya kwanza kabisa ni jambo njema sana. Natumai tunaweza kuketi na kunywa kinywaji pamoja. Usione haya mtoto,” alimwambia.

Baadaye, amejitetea na kusema alikuwa tu anafanya mzaha.

Chris Gayle alipokua akihojiwa na mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Ten Sport, Mel McLaughlin

Chris Rogers, aliyekuwa nahodha wa Sydney Thunder wakati Gayle alikuwa mchezaji wa kawaida ameambia shirika la habari la ABC Grandstand kwamba hajashangazwa na kitendo hicho cha Gayle.

Klabu ya Melbourne Renegades imesema matamshi hayo yalikuwa hayafai kabisa na yalikuwa ya “kuvunja heshima”.

Maafisa wa klabu hiyo wameomba radhi kwa McLaughlin na umma pia.

Pesa kutoka kwa faini aliyotozwa mchezaji huyo zitakjabidhiwa wakfu wa McGrath unaosaidia watu wanaotatizwa na saratani ya matiti.

Njia Ya Kucheza Fainali Ya Capital One Cup Kusakwa Leo Na Kesho
Mbwana Samatta Kwenda Nigeria Na Katibu Wa TFF