Uongozi wa klabu ya Manchester City, umeonyesha kuwa na matumaini makubwa ya kumsajili kiungo kutoka nchini Ubelgiji Kevin De Bruyne, baada ya kukaribia kiasi ambacho kilitajwa na viongozi wa klabu ya VfL Wolfsburg ya huko nchini Ujerumani.

Man City, wamejinadi kuwa na kiasi cha paund million 46 ambacho kinakaribia million 50 zinazohitajika kwa ajili ya kumng’oa De Bruyne huko Volkswagen Arena.

City, wamekua na hamu ya kutaka kumuona kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 akirejea nchini England, lakini mara kadhaa walikua wakikwamishwa na viongozi wa Wolfsburg ambao wameshikilia msimamo wa kuhitaji kiasi cha pauind million 50.

Hata hivyo mpaka sasa uongozi wa klabu hiyo ya nchini Ujerumani haujazungumza lolote na huenda hii leo wakatoa jibu la kufanya biashana na viongozi wa Man City ama kuendelea na msimamo wa kuhitaji kiasi cha pesa walichokianika hadharani tangu mwanzo.

Taarifa nyingine zinadai kwamba Man City, wanajipanga kulazimisha biashara ya usajili wa De Bruyne kufanyika ndani ya juma hili, ili kumuwezesha meneja wao kutoka nchini Chile, Manuel Pellegrini kumtumia kiungo huyo wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England wa mwishoni mwa juma hili ambapo Chelsea watasafiri kuelekea Etihad Stadium.

TP Mazembe Kuwasajili Watanzania Wengine
Tume Ya Taifa Kuchunguza Taarifa Za Ukusanyaji Vitambulisho Vya BVR Vya Askari