Beki wa Young Africans Dickson Job, amesema wanatambua uimara wa USM Alger wakiwa nyumbani hivyo watawakabili kwa umakini, ili kufanikisha azma ya kutwaa Ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2022/23.

Young Africans jana Jumapili (Mei 28) ilianza vibaya mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kuchapwa 2-1 nyumbani, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam huku ikiwa na nafasi nyingine ya kucheza mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa Jumamosi (Juni 03) nchini Algeria.

Baada ya mchezo huo, Beki Job alisema wamekubali wamepoteza mchezo dhidi ya wageni wao USMA, lakini wanakwenda kujipanga huku wakitambua namna wapinzani wao wanavyofanya wakiwa nyumbani kwenye mechi zao kwa kuwa walipata muda wa kuwatazama.”

“Tulipata muda wa kuangalia mbinu zao ambazo wanazitumia wakiwa nyumbani nasi tunafaya maandalizi kuwakabili kwani malengo ni kupata matokeo kwenye mechi ambazo tunacheza.”

“Mashabiki tunawaomba wazidi kutuombea dua na kuwa pamoja nasi kwani malengo yetu ni kupata matokeo mazuri ili tuchukue taji.”

“Kwa mchezo huu wa hapa Dar es salaam tunakubali tumepoteza, tunaamini kama wao wameweza kushinda hapa kwetu bado hata sisi tunaweza kushinda tukiwa katika Uwanja wao, Mashabiki wetu wasife moyo kwa sababu lolote linaweza kutokea tutakapokuwa ugenini.” alisema Job

Kabla ya mchezo wa jana Jumapili (Mei 28) kuanzia hatua ya makundi Dickson Job alikuwa amecheza jumla ya mechi 9 akivuja jasho kwenye dakika 806 na yupo kwenye orodha ya nyota wenye kadi ya njano ilikuwa mchezo dhidi ya Marumo Gallants alionyesha kadi ya Njano dakika ya 45 na jana alioneshwa kadi ya Njano katika Uwanja wa Mkapa.

Tunatambua mchango wa Nimrod Mkono - Serikali
Erdogan asifu ushindi wake kama ushindi wa demokrasia