DJ D Ommy wa Clouds FM, amepiga hatua nyingine kwa kuhakikisha mashabiki wake wanamiliki ladha ya kazi zake kwa urahisi kupitia ‘App’ ya simu za kisasa (androids).

DJ huyo ambaye ni mshindi wa tuzo za AFRIMMA na Africa Entertainment Awards (AEA-USA) ameibatiza App hiyo ‘Washawasha’, ikiwa ni moja kati ya majina ya Mixx zake kali alizowahi kutoa.

“Nimesogea karibu zaidi na mashabiki na wadau wa muziki kupitia App hii ya ‘WashaWasha’. Ndani yake unaweza kupata mix zangu zote, profile yangu, habari zinazonihusu na pia mtu anaweza kufanya booking,” Dj D Ommy ameiambia Dar24.

Kuipata App hiyo, mtumiaji wa simu za kisasa anapaswa kuingia kwenye ‘Google Play’ na kutafuta ‘Washawasha’.

DJ D Ommy amewahi kuachia mixing kali zikiwemo ‘The Return of the Transform Master’, ‘Kachumbali Flavor’, ‘Valentine Heartfelt’ na nyingine.

Ripoti: Mkate, chips zinazoandaliwa hivi husababisha Saratani
Guedes Kurithi Nafasi Ya Memphis Depay Old Trafford