Vuguvugu la uchaguzi likiendelea Nchini Kenya viongozi wa UDA wanashinikiza Naibu Rais William Ruto kumteua Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro kuwa mgombea.
Ruto aliwaomba wakaazi wa Kiharu kumruhusu Nyoro kutembea naye nchini kutafuta kura ili kuunda serikali ijayo
Baadhi ya viongozi wa UDA sasa wanashikiza Naibu Rais William kumteua Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro kuwa mgombea mwenza Ruto ameowaomba wakaazi wa Kiharu kumruhusu Nyoro kutembea naye nchini kutafuta kura ili kuunda serikali ijayo
Wakiongozwa na Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua, viongozi hao ambao walikuwa wamendamana na Ruto katika ziara yake kaunti ya Murang’a, walimsifia Nyoro wakimtaja kuwa mwanasiasa mwenye uwezo na ambaye amemuunga mkono Ruto bila kutikisika.
Awali, Gachagua alisema kuwa nafasi hiyo ilikuwa imetengewa jamii ya Mlima Kenya na kwamba wandani wao walijua hilo Baadhi ya viongozi katika chama cha UDA sasa wanapendekeza Naibu Rais William Ruto kumteua Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro kuwa mgombea mwenza wake.
“Ndindi amethibitisha kuwa kiongozi bora na akipata nafasi, atakuwa na uwezo wa kulihudumia taifa bora zaidi. Rekodi yake ya maendeleo unajizungumzia. Inaonyesha ana uwezo wa kutenda,” Gachagua alisema.
Katika kile kilichoonekana kuashiria ombi la viongozi hao, Ruto alisema kuwa Ndindi ni mmoja wa wafuasi wake sugu na kwamba amekuwa akisaidia kuwashawishi vijana kujiunga na kambi yake.
“Ninajua watu wa Kiharu hawajakuwa wakimwona hapa nyumbani na hili ni kwa sababu amekuwa akiandamana na mimi kila ninakokwenda. Ninapenda kuwahimiza kwa upole mmruhusu twende tutafute kura ili tuwe na uwezo wa kutengeneza serikali ijayo,”alisema Ruto.
Wiki chache zilizopita, Gachagua aliibua hisia mseto baada ya kusema kuwa nafasi ya naibu wa Ruto ilikuwa imetengewa jamii ya Mlima Kenya na kwamba Musalia Mudavadi (ANC) na Moses Wetangula (Ford Kenya) walifahamu hilo kabla ya kuijunga na kambi ya Ruto.