Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuna tatizo katika usimamizi wa elimu visiwani humo kiasi cha kusababisha kuwapo kwa matokeo mabaya kila mara.
Hayo yamesema na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi alipokutana na viongozi wa shule na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja.
Amesema kamati za shule zina jukumu la kuondoa hali hiyo kwa kuwabana waalimu kila wanafunzi wanapofanya vibaya ili waweze kupandisha kiwango cha ufaulu.
Aidha, amesema kamati hizo zinatakiwa kuwaita waalimu na kuwaweka ‘kitimoto’ waeleze sababu badala ya kuwaangalia wakati jahazi la elimu linazidi kuzama.
Vile vile, Makamu huyo wa Rais wa Zanzibar amesema matokeo mabaya ya mitihani ya wanafunzi yanadhihirisha usimamizi mdogo wa walimu shuleni ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Hata hivyo, Waziri wa Elimu, Riziki Pembe Juma amesema pamoja na kuwapo kwa mikakati mbalimbali ya Serikali kuinua Elimu, wazazi wana nafasi yao kufanikisha suala hilo na kwamba, walimu peke yao hawawezi kufanikisha.
Riziki amewahamasisha wazazi na walezi kila mara wajitahidi kufuatilia mienendo ya watoto wao kuanzia shuleni hadi majumbani

Nape apiga ‘stop’ zuio la TCRA kuhusu TV za mtandaoni
JPM: Majaliwa alikuwa hajui kama ni mwenyekiti kamati ya madawa ya kulevya