Wamiliki wa mtandao wa Facebook ambao pia wanamiliki mtandao wa picha wa Instagram, wametangaza marufuku mpya kwa watu binafsi kufanya matangazo ya bunduki kupitia mitandao hiyo.

Marufuku hiyo imekuja ikiwa ni wiki tatu tu tangu Rais wa Marekani, Barack Obama kutoa machozi alipokuwa akizungumzia umuhimu wa kuwepo kwa sheria mpya ya udhibiti wa umilikaji silaha za moto.

Hata hivyo, wamiliki wa mitandao hiyo wameeleza kuwa marufuku hiyo inawahusu watu binafsi pekee, lakini makampuni yaliyosajiliwa yanaweza kuendelea kufanya matangazo ya silaha kupitia mitandao hiyo yenye umaarufu mkubwa duniani kote.

Hatua hiyo ya Facebook ambayo ina watumiaji zaidi ya bilioni 1.5 imejikita katika kuhakikisha inazuia uuzwaji wa silaha kiholela kati ya watu binafsi kupitia mitandao hiyo.

 

Inasikitisha: Kijana aota 'mizizi' mikononi na Miguuni kwa kupata virusi hivi
Jenerali Mwamunyange Aimudu 'Hapa Kazi Tu' ya Magufuli, aongezwa Muda

Comments

comments