Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange amedhihirisha utendaji wa kutukuka na kuimudu vyema kasi ya Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’, jambo lililopelekea Rais John Magufuli kumuongeza kipande cha ziada.

Kwa mujibu wa Jenerali Mwamunyange, leo (Januari 30) ilikuwa siku ambayo alipaswa kustaafu lakini Rais ameamua kumuongeza muda wa mwaka mmoja kutokana na kuridhishwa na utendaji wake wake. Lakini pia, Rais hajamuona mtu mwingine kwa sasa anayeweza kuishika nafasi hiyo.

“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016,lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 30 januari,2016 hadi tarehe  31 Januari 2017,” Jenerali Mwamunyange aliwaambia waandishi wa habari alipokuwa katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), Upanga jijini Dar es Salaam.

Jenerali Mwamunyange aliteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi mwaka 2007 na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete.

Katika hatua nyingine, Jenerali Mwamunyange alieleza kuwa Rais Magufuli amemtua Meja Jenerali James Aliois Mwakibolwa kuwa Mkuu wa Kamadi ya Jeshi la Nchi Kavu, akichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu ambaye amestaafu kazi.

Wengine walioteuliwa na Rais Magufuli ni Meja Jenerali Yakub Sirakwi ambaye amekuwa  Mkuu wa chuo cha ulinzi wa Taifa (Commandant NDC), Brigedia Jenerali George William Ingram kuwa  Mkuu wa Kamandi ya jeshi la Anga, Bregedia Jeneralio M.W Isamuhyo kuwa  Mkuu wa jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Kadhalika, Bregedia Jenerali Jacob Kingu ameteuliwa kuwa   mkuu wa shirika la mizinga, Bregedia Jenerali Robison Mwanjelakuwa mkuu wa chuo cha Tiba Lugalo (MCMS), Brigedia Jeneral George Msongolekuwa   Kamanda wa Brigedia ya Tembo na Bregedia Jenerali Sylevesta M.Minjakuwa mkuu wa chuo cha ukamanda.

 

Facebook, Instagram wapiga marufuku matangazo ya Bunduki
Tundu Lissu: Wanaamini Bunge Limekuwa Hatari... Tutapambana