Shirika la ndege la Fastjet ambalo limekuwa likiongoza kwa kuasafiri wa bei nafuu wanayoimudu watanzania walio wengi huku wakipata huduma zenye ubora wa juu, limetangaza punguzo kubwa la bei kwa wasafiri wanaoenda nje na ndani ya nchi mwezi Septemba mwaka huu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Afisa mahusiano wa shirika hilo, Lucy Mbogoro amesema kuwa shirika hilo limetoa jumla ya siti 21,000 ambazo zimetengwa kwa ajili ya punguzo hilo kwa mwezi Septemba.

Lucy aliwataka wananchi wanaopanga kusafiri mwezi huo kukata tiketi zao mapema zaidi kwani kadiri wanavyowahi kukata tiketi ndivyo nauli inavyokuwa nafuu zaidi.

“Hata hivyo, kama hautaweza kuwahi zaidi ili kupata bei ya chini kabisa, bado unaweza kupata bei ya chini inayofuata,” alisema Afisa Mahusiano wa Fastjet.

Hizi ni bei/ nauli ya  punguzo hilo kwenda vituo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Nauli hizi zimejumuisha gharama ya kodi:

o   Dar es Salaam to Zanzibar (Tsh 79,000)

o   Dar es Salaam to Kilimanjaro (Tsh 79,000)

o   Dar es Salaam to Mwanza (Tsh 79,000)

o   Dar es Salaam to Mbeya (Tsh 79,000)

o   Dar es Salaam to Nairobi (Tsh 173,800)

o   Dar es Salaam to Entebbe/Johannesburg/Harare/Lusaka (Tsh 217,800)

o   Zanzibar to Johannesburg (Tsh 217,800)

o   Harare to Johannesburg ($100)

o   Harare to Victoria Falls ($38)

o   Harare to Dar es Salaam ($100)

o   Johannesburg to Harare/Victoria Falls/Dar es Salaam/Zanzibar (R1,381)

o   Nairobi to Dar es Salaam (KES 7,700)

o   Lusaka to Dar es Salaam (ZMW 1,080)

o   Entebbe to Dar es Salaam (Ush 428,800)

o   Entebbe to Kilimanjaro (Ush 428,800)

BOFYA HAPA KUFANYA ‘BOOKING’

Gareth Southgate Aukwaa Ukocha wa Muda England
Hans van Pluijm Afichua Siri Ya Kufungwa Kwa Young Africans