Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22 George Mpole amekiri kuwa na mwanzo mgumu msimu huu 2022/23, baada ya kushika dimbani mara mbili.

Geita Gold FC ilianza msimu kwa kupoteza 3-0 dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kisha ikalazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mpole amesema katika michezo hiyo amebaini mabeki wa timu za Simba SC na Azam FC walimkamia na hawakutaka kabisa kumpa nafasi, hivyo alikua na mazingira magumu ya kupambana.

Amesema anaamini hali hiyo imesababishwa na mafanikio alioyapata msimu uliopita, huku akiisisitiza anatarajia hali kama hiyo kuendelea katika michezo inayofuata.

Hata hivyo Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa yupo kwenye Kambi ya Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, amesema hana budi kubadilisha mbinu za kupambana na mabeki wa timu pinzani ili kuiwezesha Geita Gold FC kupata matokeo.

“Naweza kusema ligi ni ngumu, nafahamu kwa sasa kila tunapoingia Uwanjani wachezaji wanaocheza nafasi ya ulinzi upande wa timu pinzani wanajuwa wanakwenda kupamban ana Mpole, hii ni kutokana na nilioyafanya msimu uliopita.”

“Umakini umongezeka maradufu dhidi yangu, sina budi kupanga mbinu mpya ili kufanikisha lengo la kuendelea kufunga na kutetea nafasi ya kuwa Mfungaji Bora kama msimu uliopita.”

“Tumecheza michezo miwili hadi sasa, hatujapata matokeo mazuri, ila nina uhakika mambo yatakuwa mzuri na timu yetu itapata matokeo.” amesema George Mpole.

Mpole alimaliza kinara wa ufungaji Bora msimu wa 2021/22 akifunga mabao 17, akimuacha Mshambuliaji wa Young Africans Foston Mayele aliyefunga mabao 16.

Kaseja: Sina mpango wa kustaafu soka
Waliougua Uviko-19 hatarini kupata shida ya Ubongo