Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amepanga kumjibu Dk Wilbroad Slaa aliyemtaja kama mshenga katika zoezi la kumkaribisha Edward Lowassa ndani ya Chadema ili awe mgombea urais.

Gwajima ameeleza hayo jana wakati akiwahubiri waumini wake waliotarajia angejibu yaliyosemwa na Dk Slaa, lakini askofu huyo alidai kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kanisani kwa kuwa kanisa sio mahala pa kuzumzia mambo ya siasa.

“Leo sitazungumzia masuala hayo hapa kwa kuwa hili sio pango la wanyang’anyi ila nitazungumza na vyombo vya habari Jumanne ijayo,” alisema.

Askofu huyo aliyeeleza kuwa alipofika maeneo ya kanisa lake alipokelewa na waumini wake wakimshangilia kwa kumuita ‘mshenga…mshenga’, alisema kuwa atazungumza na waandishi wa habari kesho jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumjibu Dk Slaa.

Wiki iliyopita, Dk Slaa mbaye alikiri kuwa rafiki wa karibu wa Askofu Gwajima, alimtaja askofu huyo kuwa ‘mshenga’ huku akidai alimwambia kuwa alishuhudia maaskofu wa kanisa katoliki 30 kati ya 34 wakigawana fedha walizohongwa na mwanasiasa.

Samatta Ajimilikisha Ulaya
Kikwete: Mnahitaji Rais Mkali