Katika harakati za kusherekea sikukuu ya kuzaliwa kwa msanii wa bongo movi na mwanamitindo Jackline Wolper maarufu kama wolperstylish ambayo imeanza rasmi jana tarehe 6, kwa kutembelea kituo cha watoto yatima na kula nao chakula cha mchana.

Wolperstylish ambaye amekuja kivingine mwaka huu ambapo ataifanya sherehe hiyo kwa takribani wiki nzima.

Na leo kwa upande wa Dar es salaam atakuwa masaki Bucket akifanya hafla fupi na mashabiki wake  ambapo amemwalika ex wake Harmonize na mchumba wake Sarah kusherekea pamoja nae katika sherehe hiyo.

Wolper amehojiwa na kusema kuwa haoni wivu kuwaona wawili hao pamoja kwani ameshasonga mbele  na maisha yake na tayari anamchumba na wanapendana sana, hivyo amewaomba mashabiki wake kuja kwa wingi kwani kutakuwa na uzinduzi wa App yake ya Wolperstylish.

Ambapo baada ya sherehe hiyo kuisha Wolper na mchumba wake wataleekea Dodoma na tarehe 8 disemba watakuwa Maisha Basement kuendeleza sherehe hiyo na wasani wengine wakiwemo Country Boy na wanafunzi wa chuo.

Aidha Wolper amemshirikisha Barnaba Boy kama msanii ambaye atatumbuiza mubashara katika sherehe hiyo

 

Tunazindua Copa Dar es salaam
Bado tuna nafasi - Ninje