Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lina haki ya kuridhia au kutoridhia mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii, kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari – IGA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania – TPA, Plasduce Mbossa ameyasema hayo na kuongeza kuwa, mkataba huo ulisainiwa Oktoba 25, mwaka jana kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai.
Amesema, Mkataba huo ulisainiwa ili kuendeleza na kuboresha uendeshaji wa miundombinu ya bandari za Bahari na Maziwa Makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maegesho ya utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.
Aidha, amesema jambo hilo limeibua hofu juu ya maslahi ya Taifa kwenye mkataba huo ambapo watu wanahoji vifungu 31 vya mkataba pamoja na nafasi ya Bunge katika kufikia uamuzi.