Rais Mastaafu Hayati Benjamin Mkapa alikuwa kiongozi aliyeichukia rushwa kwa vitendo wakati akiongoza Tanzania kwa kipindi cha miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yemesemwa na katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue wakati akimuelezea Hayati Benjamin Mkapa katika Kongamano la kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha kiongozi huyo.

Ambapo amesema kuwa Hayati Mzee Mkapa kamwe hakupenda rushwa katika kipindi chote cha miaka kumi cha uongozi wake.

Amesema Hayati Mzee Mkapa aliunda Tume ya Warioba ambayo iliangalia mwenendo wa rushwa nchini, na kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na vitendo vya rushwa.

Balozi Sefue amesema sera ya Hayati Mkapa ya uwazi na ukweli ilisaidia kuonesha namna alivyoichukia rushwa na kuipinga kwa vitendo, ambapo pia alianzisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini.

Naibu Waziri ataka mkandarasi kufuata vigezo vya ujenzi wa mkongo wa mawasilino
Asukile amaliza atoka jela ya soka