Maisha ya Kiungo kutoka nchini Ubelgiji Eden Hazard ndani ya Real Madrid yamemalizika vibaya, ikiwa ni baada ya uongozi wa timu hiyo kuamua kuvunja mkataba wa nyota huyo licha ya kubakiza mwaka mmoja zaidi wa kukipiga klabuni hapo.

Mabosi hao wamefikia hatua hiyo baada ya Hazard kuwa na maisha mbaya tangu alipowasili ndani ya Madrid ambapo kwa muda mwingi amekuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha.

Nyota huyo anatarajiwa kuwa huru kujiunga na timu yoyote baada ya Juni 30, mwaka huu ambapo ndiyo itakuwa siku ya mwisho wa mkataba wake na klabu hiyo ambayo alijiunga nayo akitokea Chelsea.

Nyota huyo amekuwa akimezewa mate na baadhi ya klabu za England ambazo zinataka kumrejesha kwenye ligi hiyo kwa mara nyingine baada ya kutikisa kwa miaka kadhaa kabla hajatua Hispania.

PSSSF yatoa mafunzo elimu ya mafao kwa Jeshi la Polisi
Wanyamapori: Tanzania yavuka lengo mkakati kitaifa