Baada ya kuthibitika ameondoka Mtibwa Sugar, Kocha Hitimana Thiery amefunguka na kueleza undani wa tatizo lililomuondoa kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara msimu wa 1998/99 na 1999/2000.

Hitimana ambaye alikabidhiwa mikoba ya Zubery Katwila aliyetimkia Ihefu FC mwishoni mwa 2020, amesema amesema shida kubwa iliyopo Mtibwa Sugar kwa sasa ni kukosa wachezaji wenye uwezo wa kupambana ndani ya dakika 90 na kupata matokeo chanya.

Kocha huyo kutoka nchini Rwanda amesema asilimia kubwa ya wachezaji waliondoka klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu, walikua na uwezo mkubwa wa kupambana na kwa bahati mbaya viongozi walishindwa kujaza nafasi zao kwa kukidhi vigezo vya kiufundi.

“Walikuwa na nguvu hapo awali na walikuwa na uwezo wa kufanya vizuri ila pale ambapo wale wachezaji waliokuwa wapo kikosi cha kwanza wameondoka ilikuwa tatizo hapo na kingine ni kwamba hakujafanyika usajili mkubwa.

“Naona kwamba kikosi kitapambana kurudi kwenye uimara wake ila ni mpaka muda kidogo upite kwani hakuna kitu chepesi kwenye maisha ya mpira,” amesema Hitimana.

Kocha Hitimana akiwa Mtibwa Sugar kwenye michezo 19 ambayo walikuwa wamecheza wakati ule kabla ya usajili wa dirisha dogo alicheza jumla ya michezo 18 na alikosa mchezo mmoja dhidi ya Mbeya City msimu huu 2020/21.

TPA yadhamiria kuvunja rekodi ukusanyaji mapato
Bumbuli: Hatujaridhishwa na adhabu ya Mwakalebela