Kushindwa kwa mataifa 16 ya Afrika kuegemea upande wowote katika sakata la upigaji kura juu ya nchi ya Urusi kujitwalia maeneo ya Ukraine, kumetajwa kusababishwa na uoga wa kuhofia ukosaji wa misaada kwa nchi za ulaya zilizoendelea.
Hatua hiyo, inafuatia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, limeshutumu “unyakuaji haramu” wa Urusi kwa maeneo ya nchi ya Ukraine baada ya Moscow kupinga maandishi sawa na hayo katika Baraza la Usalama mwishoni mwa Septemba, 2022.
Nchi 26 za Afrika, zilipiga kura kuunga mkono azimio hilo la kukataa kura ya maoni yenye utata ya Moscow, katika mikoa minne ya Ukraine huku nchi nyingine 16 zikishindwa kufungamana na upande wowote.
Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ethiopia, Jamhuri ya Kongo, Afrika Kusini, Sudan, Uganda, na Zimbabwe ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zilijizuia kupiga kura, huku Eritrea, ambayo hapo awali ilipiga kura ya kukataa azimio la Umoja wa Mataifa la kulaani uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, pia ikijizuia.
Hata hivyo, inahisiwa kuwa sababu ya nchi tatu kati ya hizo kushindwa kupiga kura ni kuona aibu kwa kuwa zilimkaribisha Mkuu wa wanadiplomasia wa Urusi Sergei Lavrov, wakati wa ziara yake katika maeneo ya nchi hizo, mapema mwezi Julai, 2022, ambapo Burkina Faso, Kamerun, Guinea ya Ikweta, na Sao Tome hazikuwepo katika kusanyiko hilo la Baraza Kuu la nchi wanachama 193 lililokuwa limekutana katika mkutano wa dharura.
Ilipitisha azimio hilo kwa kura 143 za ndio, huku nchi tano zikipinga na 35 zikikataa, zikiwemo China, India, Pakistan, na Afrika Kusini, licha ya juhudi za kidiplomasia za Marekani na majimbo matano yaliyopiga kura dhidi yake ni Urusi, Belarus, Syria, Korea Kaskazini na Nicaragua.
Mapema mwezi huu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alizuru barani Afrika katika juhudi za kukabiliana na uwezekano wa Urusi kushikilia bara hilo , lengo likuwa ni kuwashawishi viongozi waunge mkono Kiev na alilazimika kukatiza ziara yake baada ya Moscow kuzidisha mashambulizi yake kwa nchi yake.