Profesa wa Chuo cha Ki-kristo cha Wheaton College, kilichoko Chicago nchini Marekani ametimuliwa kazi kufuatia tamko lake kuwa Wailslam na Wakristo wanaabudu Mungu mmoja.

Awali, Profesa huyo aliyetajwa kwa jina la Larycia Hawkins alimaishiwa kazi baada ya kuandika kwenye mtandao wa Facebook akihusisanisha tamko la Papa Francis na kile alichokiamini.

As Pope Francis stated last week, we worship the same God,” ilisomeka sehemu ya maandishi ya profesa huyo ambayo yalimharibia kazi.

Uongozi wa Wheaton walisema kuwa wamekwazwa na post ya Profesa huyo kwa kuwa inakanganya mafundisho ya kiimani ya chuo hicho.

Hata hivyo, awali Profesa huyo na uongozi wa chuo hicho walitoa tamko la pamoja kuwa wameamua kuachana kwa wema.

 

Video: Beyonce alivyonusurika ajali Jukwaani kwenye Super Bowl
Picha: Angelina Jolie ‘Akwanguliwa’ Tena Mgongoni Akiandaa Filamu Mpya