Israel imewawekea vikwazo vya kusafiri wabunge wawili wa chama cha Democratic nchini Marekani baada ya Rais Trump kuiomba nchi hiyo kufanya hivyo.

Rais Trump amesema kuwa Israel itaonyesha udhaifu mkubwa kama itawaruhusu wabunge hao ambao ni IIhan Omar na Rashida Tlaib kutembelea taifa hilo.

Hatua hiyo inakuja mara baada ya tamko la balozi wa Israel nchini Marekani mwezi uliopita kwamba wabunge hao wawili hawataruhusiwa kuitembelea nchi hiyo.

Taarifa hiyo imethibitishwa na wizara ya mambo ya ndani ya Israel ambapo imesema kuwa mpaka sasa haielewi ni kwanini wabunge hao wanaoupinga utawala wa Trump wamezuliwa kuingia nchini humo.

Aidha, Rais Trump ambaye ana uhusiano wa karibu na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ametofautiana na wabunge hao kutokana na kauli tata ya kibaguzi aliyotoa dhidi yao, ambapo aliwataka wabunge hao warudi katika mataifa yao waliyotoka familia zao.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani, viongozi hao wawili walikuwa na ziara ya kikazi Jumapili ya wiki hii, ambayo pia ingejumuisha wao kufika eneo tata la Temple Mount jijini Jerusalem, linalotambuliwa na Waislamu kama Haram al-Sharif.

Hata hivyo, ziara ya ukingo wa Magharibi ilipangwa na shirika la Miftah, linaloongozwa na mpatanishi wa amani wa Palestina, Hanan Ashrawi.

 

 

Simbachawene ang'aka, 'Kwani mmelazimishwa kununua?
LIVE: Ziara ya Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, Mazimbu mkoani Morogoro