Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Colombia, James Rodriguez ameanza mchakato wa kusaka nyumba ya makazi mjini Manchester nchini England.

Rodriguez ameanza kufanya mchakato huo, kufuatia tetesi zinazoendelea katika baadhi ya vyombo vya habari barani Ulaya, ambazo zinadai kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka katika klabu ya Real Madrid anayoitumikia kwa sasa.

Kwa mujibu wa jarida la michezo la Don Balon la nchini Hispania, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, tayari ameshaiweka sokoni nyumba yake ya mjini Madrid.

Harakati za Rodriguez kusaka nyumba mjini Manchester, zimepokelewa kwa mtazamo tofauti, miongoni mwa wadau wa soka duniani, ambapo baadhi yao wanahisi huenda akajiunga na Man City huku wengine wakielekeza fikra zao Man Utd.

Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa Rodriguez, akajiunga na Man Utd ambayo msimu ujao itakua chini ya meneja kutoka nchini Ureno, Jose Mourinho.

Rodriguez, ameonyesha kushindwa kumshawishi meneja wa Real Madrid,  Zinedine Zidane, katika harakati za kumtumia mara kwa mara kikosini mwake, hali ambayo inaendelea kutoa msukumo wa kuamini kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka wakati wa majira ya kiangazi.

Jurgen Klopp Adhamiria Kumsajili Sadio Mane
Wakimbizi 200 wa Boko Haram Wafa kwa Njaa