Bench la ufundi la Azam chini ya makocha wa Hispania limeamua kumpunguza kipa raia wa Ivory Coast katika orodha ya wachezaji wanaowania kusajiliwa na klabu katika msimu mpya.

Daniel Yeboah ambaye ni kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast alikuja nchini kwa majaribio lakini ameshindwa kulishawishi benchi la ufundi la Azam chini ya Zeben Hernandez hivyo kusitisha majaribio yake.

Wakati Yeboah akisitishwa kuendelea na majaribio, kipa mwingine raia wa Hispania, Juan Jesus Gonzalez ameendelea na majaribio ya kuwania kusajiliwa.

Gonzalez alichezesheshwa dakika 45 za kwanza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ashanti United iliyopigwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Chamazi. Alijaribiwa mara moja tu kwa krosi aliyoipangua vizuri.

Kocha Hernandez aliomba kuwatathmini wachezaji wa zamani, wapya na wale waliokuwa wametolewa kwa mkopo ili kuamua nani anastahili kuvaa uzi wa Azam msimu mpya.

Majibu Ya Vipimo VYa Demba Ba Yawekwa Hadharani
Tatu Zathibitisha Ushiriki Wa Klabu Bingwa Duniani