Picha za X-ray imeonyesha, mguu wa kushoto wa mshambuliaji kutoka nchini Senegal, Demba Ba amevunjika mfupa wa ugoko na huenda ikamchukua muda kupona jeraha hilo.

Ba, alikimbizwa hospitali baada ya kupatwa na maswahibu hayo akiwa katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini China, ambapo klabu yake ya Shanghai Shenhua ilikua ikipapatuana Shanghai SIPG ambao mwishowe walikubali kupoteza kwa kufungwa mabao mawili kwa moja.

Wakati Ba akipatwa na majeraha ya kuvunjika mguu, Shanghai Shenhua walikua nyuma kwa bao moja kwa sifuri.

Picha ya X-Ray inayoonyesha jeraha la Demba Ba

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, alipofikisha hospitali lipatiwa matibabu ya awali na kupewa dawa za usingizi ambazo zilimchukua muda wa saa nne kabla ya kuamka.

Daktari anayemtibu Ba, alisema kwamba swali la kwanza alilouliza mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kucheza soka katika ligi ya nchini England lilikuwa ni kutaka kufahamu matokoe ya mchezo aliouacha ukiendelea.

“Tumeshinda mchezo wetu?” hivyo ndivyo alivyoniuliza, alisema daktari huyo

Naibu meya wa jiji wa Shanghai Zhao Wen alipomtembelea Ba hospitali

Mwenyekiti wa klabu ya Shanghai Shenhua, Wu Xiaohui alifika hospitalini hapo kumjulia hali Ba, baada ya kuzinduka kutoka usingizi na amemtakia kila la kheri katika kipindi hiki cha kujiuguza jeraha lake.

Katika hatua nyingine mchezaji aliyemvunja Ba, Sun Xiang naye alifika hospatali kumjulia hali, pamoja na naibu meya wa jiji wa Shanghai Zhao Wen.

Ukimya wa Msanii Hamisi Amani Kujibiwa leo Mchana
Juan Jesus Gonzalez Aendelea Kupeta Azam FC