Meneja wa Msanii Diamond Platnum ametoboa siri kwamba mama mzazi wa msanii huyo na mchumba wake Tanasha Donna wamezaliwa tarehe na mwezi mmoja ambapo Julai 7 mwaka huu kutafanyika tukio ambalo halijawekwa wazi litakuwa ni lipi.

Msanii huyo alipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita alitangaza msimu wa pili wa tamasha la wasafi sambamba na tukio kubwa litakalo fanyika Julai 7,2019 alilodai litafanyika maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam Tanzania.

”Ni kweli siku hiyo kutakuwa na tukio kubwa kwa msanii wetu Diamondi ambapo ni siku ya kuzaliwa kwa Mama yake Sandra na mchumba wake Tanasha Donna ambao wote wamezaliwa Julai 7 kasoro miaka tofauti amesema” Babu Tale.

Babu Tale ameongeza kuwa pamoja na kwamba ni siku ya kuzaliwa kwa wapendwa wake hao lakini pia lolote linaweza kutokea,ikiwemo ndoa ambayo mashabiki wake wengi wanahisi hivyo ila tusubiri muda utakapofika.

 

Membe akerwa na suala la utekaji, 'Lisipokemewa litafika mpaka kwenye uchaguzi'
Tanzania yaingia kwenye rekodi mpya AFCON

Comments

comments