Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Jakaya Kikwete anatarajia kuiachia nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho na Kumkabidhi rasmi Rais John Magufuli hivi karibuni.

Hayo yamebainika baada ya Dk. Kikwete kutangaza rasmi jana alipokuwa anaongea na wazee wa Manispaa ya Singida kuwa sherehe za maadhimisho ya ya miaka 39 zinazofanyika leo mjini Singida, zitakuwa sherehe zake za mwisho akiwa Mwenyekiti wa Chama hicho.

Endapo Dk. Kikwete ataachia nafasi hiyo mwaka huu, itakuwa mapema zaidi kama walivyofanya watangulizi wake kwani kalenda ya Chama hicho inaonesha kuwa Mkutano Mkuu wa kumpata Mwenyekiti mpya utafanyika mwaka 2017.

Kadhalika, Kikwete alionesha kufurahishwa na ushiriki wake katika sherehe hizo mjini Singida akihitimisha kukiongoza chama hicho kwa kuwa ndio mji ambao alianza kuwa kiongozi mwaka 1975, alipokuwa Katibu Msaidizi wa Tanu wilaya ya Singida Mjini.

Aliwashukuru wazee wa mji huo kwa busara zao wakati wa michakato ya kumpata mgombea urais mwaka jana akikiri kuwa uliuwa uchaguzi mkumu mno na kwamba bila busara zao mambo yangekuwa tofauti na yalivyo sasa. Pia, akiwaomba kuendelea kuunga mkono Serikali ya CCM katika kuleta maendeleo.

“Niwaombeni ninyi wazee na wakazi wote wa Mkoa wa Singida, muiunge mkono Serikali hii ya awamu ya tano inayoonesha dalili nzuri katika kutekeleza mambo yake,” alisema Dk. Kikwete.

Mifuko ya Jamii yabanwa koo
Mbowe anamng'ata na Kumpuliza Zitto? aeleza sababu ya kumtosa Uwaziri Kivuli