Msanii mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Judith Wambura maarufu kama Lady JayDee yupo kwenye hatari ya kufungiwa kwa wimbo wake mpya wa ‘One Time’ baada ya kutuhumiwa kuhamasisha matumizi ya uvutaji wa Bangi.

Mashairi ya wimbo huo yamelalamikiwa na mashabiki wa muziki wa bongo fleva kuwa na maneno yanayo hamasisha uvutaji wa bangi.

Kwa mujibu wa mtandao wa kijamii wa Jamiiforums umeandika kuwa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), limethibitisha kupokea kwa malalamiko kutoka kwa wadau wa muziki, kuhusu mashairi ya wimbo huo.

Tuzo za BET zamuibua Octopizzo

Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza amesema wanaendelea kufanya uchunguzi wa kisheria kuhusiana na nini hasa dhumuni la mistari ya Wimbo huo aliouachia Septemba 14, 2020.

Papa Francis ataka utaratibu mpya wa ulimwengu
Sita wafariki kwa dhoruba Mexico