Tuzo za  BET  siku ya jana wametangaza vipengele 17 vya tuzo 15 za (BET Hip Hop Awards), ambazo zimetajwa kuoneshwa Oktoba 27 mwaka huu.

Afrika Mashariki imepata mwakilishi kwenye tuzo za mwaka huu,amabye ni rapa Khaligrah Jones kutoka Kenya, ametajwa kwenye kipengele cha ‘Best International Flow’ akichuana na wakali toka Ufaransa, Uingereza, Brazil na Afrika Kusini inayowakilishwa na Nasty C.

Hata hivyo mara baada ya Khaligraph Jones kutajwa na BET,  kumemuibua rapa Octopizzo  kutoka nchini Kenya ambaye ni hasimu wa muda mrefu wa msanii huyo.

Msanii Octopizzo ametumia ukurasa wake wa Twitter kumpongeza hasimu wake khaligraph_jones ambapo ametumia nafasi hiyo kuwasihi mashabiki zake kumpigia kura rapa huyo baada ya kutajwa kwenye tuzo hizo kubwa na maarufu Duniani.

“We’ve always had our differences & that will remain like that. But Congratulations Brayo aka KJones on your BET nomination, All my die hard go vote for jones, na akishinda hio award namvutisha vela Cha lazima si ati nini.

Wanaowarubuni wapiga kura wapewa onyo
Mosimane awatema Masandawana

Comments

comments