Mabingwa wa soka nchini England, Leicester City huenda wakamuweka sokoni kiungo wao kutoka nchini Algeria, Riyad Mahrez baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya.

Leicester City tayari wameshakamilisha mpango wa kumuuza kiungo kutoka nchini Ufaransa N’Golo Kante ambaye mwishoni mwa juma lililopita alijiunga na Chelsea, baada ya kugoma kusaini mkataba mpya.

Suala la kugoma kwa Mahrez kwa kigezo cha kutoridhishwa na mshahara wa Pauni 100,000 kwa juma, ufumbuzi wake unatarajiwa kutatuliwa na mpango wa kumuweka sokoni ili kusaka pesa ambazo zitatumika kumsajili mbadala wake huko King Power Stadium.

Hata hivyo kabla ya Mahrez kushindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya, tayari alikua ameshaonyesha ya kutaka kuondoka klabuni hapo kwa kigezo cha kusaka mahala pengine ambapo patampa changamoto tofauti.

Leicester City, walimsajili Riyad Mahrez mwaka 2014 akitokea nchini Ufaransa katika klabu ya Le Havre kwa ada ya Pauni 375,000, na msimu uliopita alichangia kwa kiasi kikubwa kuipa ubingwa wa kihistoria The Foxes.

Video: Demba Ba Avunjika Mguu Akiwa Vitani
Massimiliano Allegri Aikebehi Man Utd Kwa Kivuli Cha Pogba