Mshambulizi kutoka nchini Senegal, Demba Ba amevunjika mguu akiwa katika majukumu ya kuitumikia klabu yake ya Shanghai Shenhua inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini china.

Ba mwenye umri wa miaka 31, alipatwa na mkasa wa kuvunjia mkuu wake wa kushoto alipokua akikabiliana na beki wa Shanghai SIPG mita chache tu kabla ya kuingia katika eneo la harati (Kisanduku cha hatua 18).

Video ya mchezo huo imesambaa katika mitandao ya kijamii na inaonyesha tukio hilo ambalo linaogopesha kutokana na mguu wa Ba, kuonekana dhahir ulivunjika zaidi ya mara moja.

Kocha wa klabu ya Shanghai Shenhua, Gregorio Manzano alisema kwa uchungu kuwa, tukio hilo linaweza kumlazimisha nyota huyo kustaafu kucheza soka.

Kwa msimu huu wa ligi ya nchini China, Ba anaongoza katika orodha ya wafungaji akiwa na jumla ya mabao 14 katika michezo 18 aliyocheza.

Ba aliwahi kuzitumikia klabu za nchini England kama West Ham, Newcastle na Chelsea kabla ya kuelekea nchini China akitokea Uturuki katika klabu cha Besiktas ambayo ilikubali kumuachia kwa ada ya Pauni milioni 12.

Paul Makonda Amjibu Meya wa Dar es salaam
Leicester City Kumuweka Sokoni Riyad Mahrez