Mwanamuziki maarufu wa Hip Hop Mabeste ametoa ufafanuzi juu ya kile kinachoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusu taarifa za kukimbiwa na mke wake ”mama Kendrick”.

Mabeste amesema hajui kinachoendelea kuhusu taarifa hizo na hata yeye ameona tarifa hizo katika kurasa za habari za udaku na mitandao ya kijamii.

Ambapo taarifa zinadai kuwa Mabeste amekimbiwa na mke wake kwa sababu ya shida na matatizo na sasa hivi yupo mjini Moshi akiwa na mwanaume mwingine.

“Inawezekana ila sijajua kwa sasa hivi, ikifikia hatua ya kutengana watu watajua na hata wasipojua ni sawa kwa sababu katika maisha, kutengana na kuanzisha mahusiano mengine ni moja ya maisha ni vitu vya kawaida”, amesema Mabeste.

Ameendelea kwa kusema kuwa suala hilo halina ukweli wowote, na hata akikimbiwa ni sawa tu maana hatakuwa wa kwanza wapo wengi waliokimbiwa na wapenzi wao na maisha yakaendelea na lolote litakalo kuja mbele yake atashukuru na ataendelea mbele.

Katika hatua nyingine Mabeste amesema kuwa alijitoa kuhangaikia maisha ya mke wake kipindi alipokuwa matatizo ya maradhi, alifanya vile kwa sababau ya upendo tu na majukumu kama mtu wake wa karibu na wala ahitaji fadhila yoyote .

Video: Kwanini mwanadamu amekatazwa kuzini ?
Disemba 31 laini zote zisizosajiliwa kufungwa, NIDA, TCRA waungana kufanya usajili